Siku nne kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la Mataifa Ulaya EURO 2024, timu ya Taifa ya Uholanzi imepata pigo baada kiungo wake Frenkie de Jong kuripotiwa kuwa atakosa michuano hiyo kutokana na kutokuwa fiti baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu.

De Jong alikosa mechi za wiki za mwisho za msimu wa 2023/24 za klabu yake ya Barcelona kutokana na tatizo kwenye kifundo cha mguu hali inayomfanya aikose michuano ya EURO 2024 inayotarajiwa kuanza kurindima kuanzia Juni 14 nchini Ujerumani. 

Kambi ya Uholanzi imekuwa ikifanya kazi ya kumfanya de Jong kuwa fiti kwa ajili ya kuanza kwa mashindano huku kiungo huyo wa zamani wa Ajax akikiri kuwa yuko tayari kuhatarisha utimamu wake kwa kucheza Euro 2024 lakini sasa imeshindikana.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement