NYOTA wa Braga, Armindo Tue Na Bangna (Bruma) ameweka rekodi ya kuivaa jezi namba saba ya timu ya taifa ya Ureno ambayo imevaliwa na Staa wa Al Nassr tangu mwaka 2007.

Ronaldo ambaye hajajumuishwa kwenye kikosi cha Ureno cha Kocha Roberto Martinez kilichokabiliana na Swesen kwenye mchezo wa kirafiki wa ushindi wa mabao 5-2, ameivaa jezi hiyo kwa takribani miaka 18 na aliomba asijumuishwe kikosini kwa ajili ya mchezo huo.

Katika mchezo huo uliopigwa wikiendi Bruma aliweka historia hiyo, huku pia akitupia bao dakika ya 57 kutokana na pasi nzuri ya nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes.

Hata hivyo, inaelezwa nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid amevaa jezi namba saba kwenye vikosi vyote alivyocheza kwa miaka 22 na kujiweka kwake pembeni ili apumzike na familia yake na alihofia asije akapata majeraha ambayo yanaweza kumzuia kucheza Euro 2024 na ataitumia jezi yake hiyo.

Jezi hiyo amepewa Bruma mwenye umri wa miaka 29 ambaye msimu huu ameonyesha kiwango bora akifunga mabao manane na kutoa asisti sita katika mechi 30 za michuano yote.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement