NYOTA MCHANGA WA REAL MADRID ARDA GULER "MESSI WA UTURUKI" AMEKUWA MCHEZAJI MDOGO ZAIDI KUIWAKILISHA TIMU YAKE YA TAIFA
Tangu ajiunge na timu hiyo, kiungo mshambulijai wa Real Madrid, Arda Guler amekuwa akionesha kiwango kizuri cha soka baada ya kusajiliwa na miamba hao wa Hispania na Ulaya kutoka Fenerbahce.
Baada ya kutua jiji la Madrid msimu uliopita wa joto, Arda mwenye umri wa miaka 19, amekuwa na mchango muhimu kwenye timu hiyo. Kipaji cha kinda huyo kutoka Ankara, Uturuki, kilionekana mapema kabisa toka akiwa shule ya msingi na sasa ndiye gumzo katika ulimwengu wa soka.
Arda Guler, ni mchezaji mchanga zaidi kuifungia Uturuki, na mchezaji wa tatu mwenye umri mdogo zaidi kuiwakilisha timu ya taifa ya Uturuki.