NIGERIA, SENEGAL, MORROCO ZAPIGA HATUA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE FIFA U17 2024
Nchini Ethiopia, Vijana wa Burundi Starlets waliizaba Djibouti 18-0 huku nyota wazoefu Habonimana na Roy Nzoyikorera wakifunga mabao 13 kati yao.
Habonimana aliweka rekodi ya historia kwa kufunga mabao saba, akitikisa wavu katika dakika ya 7, 52, 57, 66, 70, 82 na 86.
Aidha, nyota mwenza Nzoyikorera naye alifunga mabao sita baada ya kufungua bao kwa sekunde 55 na kufunga tena baadaye dakika ya 11, 34, 45, 48 na 72.
Ushindi huo muhimu kwa Burundi, unajiri huku timu hiyo ikiendelea na fomu nzuri ya kuvutia katika mechi hizi za kufuzu, baada ya kuicharaza Botswana 4-1 na 20 katika raundi ya awali.
Burundi imeweka mguu mmoja katika hatua ya mzunguko wa mwisho wa kufuzu, huku wakitarajiwa kuchuana na Ethiopia au Kenya katika nafasi ya Kombe la Dunia la Wanawake U17 litakalopigwa Jamhuri ya Dominika baadaye mwaka huu.
Nigeria, Senegal, na Morocco nazo zimepiga hatua kubwa kuelekea Kombe la Dunia kwa Wanawake Fifa U17 2024, kwenye mechi za kufuzu zingine zilizofanyika wikendi hii.
Mjini Bamako, Mali, Flamingo wa Nigeria waliondoka na pointi muhimu dhidi ya Burkina Faso kwa kutoka sare 1-1 ugenini dhidi ya Burkina Faso Jumamosi.
Senegal nao walichukua uongozi wa mabao mawili katika jitihada zao za kufikia raundi ya mwisho, huku wakishinda Liberia 3-1 kule Thiès.
Wawakilishi wa Afrika kwenye Kombe la Dunia la Wanawake Chini ya Miaka 17 watajulikana mwishoni mwa mzunguko wa nne wa mwisho wa kufuzu mwezi ujao.