NGOMA AWATOLEA UVIVU MASHABIKI SIMBA
Mastaa wa Simba wanaingia kambini leo kujiandaa na mechi ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast itakayopigwa Novemba 25, jijini Dar es Salaam,
Tangu kipigo cha mabao 5-1 ilichopewa na Yanga katika mechi ya watani ya Kariakoo Derby, Simba hali ni kama haijatulia kwa mabosi wa klabu hiyo kujifungia kwa siku zaidi ya mbili wakipanga mikakati baada ya kuwafuta kazi makocha watatu kwa mpigo akiwamo kocha mkuu, Roberto Oliveira 'Robertinho.
Pia mitaani hadi kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa Wanasimba wakiushutumu uongozi na hata wachezaji,
lakini sasa mastaa wa timu hiyo wameamua kuvunja ukimya na kuwatuliza kwa kuwaambia; "Tulieni, tumewasikia na tunajipanga kuwapa raha zaidi.!
Kauli hiyo imetolewa na kiungo Fabrice Ngoma na nahodha msaidizi, Mohamme Hussein Tshabalala', waliosema kwa nyakati tofauti kuwa, hata wao wanaumia kwa kilichotokea Novemba 5, na sasa wanajipanga upya ili kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo kwa mechi za CAF na zile za ligi ya ndani.
Ngoma, aliyesajiliwa msimu huu akiwa mmoja ya wachezajill wapya, alisema
kwa uzoefu wake wa soka la Afrika, presha za namna hiyo huwa zipo sana alipitia hivyo akiwa Raja Casablanca lakini anajua namna ya kukabiliana nazo na kuzishinda.
"Mara nyingi mashabiki wanataka matokeo mazuri tu, na ni haki yao lakini wanatakiwa kutambua soka lina matokeo matatu, kushinda, kutoa sare na kupoteza. Tunajua namna mashabiki wetu wameumia lakini haina budi kutoa lawama kwa yeyote yule, tunatakiwa kuungana kuwa kitu kimoja na naamini tutarejea kufanya vizuri kwani bado tupo kwenye msitari na kila kitu kinawezekana," alisema Ngoma ambaye
alitajwa na Robertinho, kama usajili bora wa msimu huu sambamba na beki Che Malone Fondoh.