NBC CHAMPIONSHIP LEAGUE: KLABU YA BIASHARA UNITED NDIO TIMU ILIYOFUNGA MAGOLI MENGI HUKU PAMBA JIJI FC IKIRUHUSU KUFUNGWA MAGOLI MACHACHE
KLABU ya Biashara United Fc ndiyo timu ambayo imefunga magoli mengi zaidi mpaka sasa kwenye ligi bora ya NBC Championship.
Biashara United Fc imefunga jumla ya magoli 55 mpaka sasa katika jumla ya mechi 28 walizocheza mpaka sasa kwenye ligi ya NBC Championship League.
Biashara United wiki hii watacheza dhidi ya Pan African Fc katika mehi za muendelezo wa NBC Championship katika dimba la Mej. Gen. Isamuhyo.
Pamba Jiji Fc ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya NBC Championship ndiyo timu ambayo imeruhusu magoli machache zaidi katika mechi ishirini na nane (28) walizocheza mpaka sasa.
Pamba Jiji Fc wameruhusu jumla ya magoli 16 pekee na mpaka sasa zimesalia jumla ya mechi mbili (2) pekee ligi ya NBC Championship kutamatika.