Msimu huu wa ligi ya NBC championship 2023/2024 tumeona timu zikijitahidi kufamania nyavu kwel kwel maana tuliona timu ya biashara UTD ikiwa ndo timu iliyofunga mabao mengi takribani mabao 60 lakini ndio ilikua timu iliyo shinda mabao mengi kwenye Mchezo mmoja dhidi ya Ruvu shooting FC.

Ukienda pale EPL msimu huu 2023/2024 ulio tamatika hivi punde tumeshuhudia jumla ya mabao 1246 yakifungwa na timu 20 zilizo shiriki ligi hiyoo, kwa mantiki hiyoo sasa ni NBC championship league mabao 576 lakini pale EPL mabao 1246.

Mbali na record hiyoo ya magoli 576 pale NBC championship league 2023/2024 pia tumeshuhudia msimu ambao umetoa timu iliyo kusanya points nyingi Zaidi kuliko misimu yote iliyo pita na timu hiyo ni Ken gold SC iliyo fikisha points 70 lakin pia kutoa mfungaji bora Edger William magoli 21 na goli kipa mwenye cleansheets nyingi Zaid Casto Mhagama akiwa nazo 19.

Ubora wote huu wa ligi ya NBC championship league misimu huu wa 2023/2024 unaweza sema umechagizwa Zaidi na uwekezaji kutoka bank ya taifa ya biashara NBC pamoja na Tv3 ambao wamepelekea wachezaji kujituma,viongozi kuongoza timu vizuri kwa kufanya uwekezaji mkubwa na tumeona mafanikio makubwa Sanaa kwa baadhi ya klabu kuuza wachezaji kwenda ligi kuu ya NBC na kufanya baadhi ya wachezaji kuongeza ubora mkubwaa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement