NBC: BODI YA LIGI KUWAANDALIA YANGA SC SHEREHE ZA UBINGWA WA LIGI KUU
Mdhamini Mkuu wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara , Championship na Ligi ya Vijana (NBC Youth League) bemki ya NBC imetangaza kushirikiana na Shirikisho la Soka nchini (TFF) sambamba na Bodi ya Ligi kwaajili ya kuandaa Sherehe za kukabidhi Ubingwa wa Klabu ya Yanga 2023/24 Mei 25 mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma cha NBC Godwin Semunyu ameeleza kuwa wamendelea kuonyesha dhamira yao katika maendeleo ya michezo ambapo mbali ya kuwekeza zaidi ya bilion 32.6 jambo ambalo halijawahi kufanyika kwenye soka lakini wamesaidia katika kutengeneza ajira.
“Niwapongeze kwanza Young Africans kwa kuwa Mabingwa wa mwaka 2023/24 ambao ni msimu wa tatu mfululizo na Mara 30, Sisi kama Benki ya NBC tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaboresha soka la Tanzania kwa kutoka zaidi ya bilion 32.6 kwa miaka mitano ambayo ni uwekezaji mkubwa kabisa kutokea kwenye michezo Tanzania, uwekezaji ambao ni zaidi ya Ligi kuu lakini imehusisha NBC Championship na Ligi a viajana ambayo ni NBC Youth League, “ Godwin Semunyu - Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya UMMA.
Kwa upande wake Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe ameeleza kuwa siku ambayo imepangwa kwa wao kukabishiwa kombe hilo kwa maana ya Mei 25 katika mchezo dhidi ya Tabora United, wanachama na mashabiki wa wakati wanaingia Uwanja wa Benjamini Mkapa majira ya saa Tano Asubuhi, NBC watakuwa wameandaa Helkopta maalumu ya kufanya Paredi ya Kombe kwa Dar es salaam nzima.
“Jumamosi ya Tarehe 25 siku ya kibingwa Asubuhi na mapema, saa Tano kamili Asubuhi wakati watu wakiwa wanaingia Benjamin Mkapa, NBC Bank wameandaa Helkopta maalumu ya kufanya Paredi ya Kombe letu Dar es salaam nzima yaani Kawe, Mbagala sijui Kigamboni, Yombo kote, Kombe la NBC Premier League msimu huu ambalo Yanga tunakwenda kukabidhiwa na lenyewe litafanya paredi la angani, na malaika huko watakuwa wanaliona Yanga hao kombe lao linapita, “
“Tarehe 25 asubuhi tunafanya paredi ya juu kwanza, ubingwa unatembea, na tumemuambia anayerusha yapo maeneo hiyo helkopta yapo maeneo inaenda juu, yapo maeneo inashuka chini, ukifika Tandika anatakiwa apande, akija mjini Kariakoo anashuka kidogo pale kwenye mataa na akiwa anakata kuja Jangwani pale kwenye ule mtaa anatakiwa ashuke zaidi, wale wakae waone mita kama tatu ikiwezekana, wafungue madirisha watazame hili ndilo Kombe la Yanga linapota, ” Afisa Habari Yanga SC – Ally Kamwe.
Ally Kamwe ameeleza kuwa mara baada ya paredi hilo, majira ya saa Tisa jioni Helkopta itatua Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo wananchi watalipokea Kombe hilo.