Simba jana iliachana na mchezaji kiraka Erasto Nyoni baada ya mkataba wake kumalizika. Simba inaendelea kupunguza wachezaji ili kusaka wapya kuziba nafasi hizo , leo Namungo wameiwahi saini yake mapema ikijiandaa na msimu ujao Ligi Kuu Bara.

Namungo ambayo imemaliza Ligi ikiwa nafasi ya tano na pointi 40 imefanya usajili wake wa kwanza kwa Erasto Nyoni wakiamini atawasaidia  kutimiza malengo yao ya  msimu ujao

Kocha wa Simba, Roberto Oliveira 'Robertinho alikuwa anamuangula zaidi kama kiongozi wa wachezaji ndani na nje ya Uwanja. Lakini apewe heshima yake, akapumzike. Simba ijayo inahitaji watu wa kazi watakaoirejesha kwenye ubora wake si kuangaliana machoni.

Nyoni mwenye umri wa miaka 35, alisajiliwa na Simba msimu wa 2017-2018 akitokea Azam akiwa sambamba na Aishi Manula, John Bocco na Shomary Kapombe na kwa misimu minne kati ya mitano aliisaidia timu hiyo kubeba taji manne la Ligi Kuu Bara, mataji mawili ASFC na kuifanya Simba itishe.

Huu ni mwake wake wa 18 dimbani tangu alipoanza kucheza Ligi Kuu mwaka 2005 katika kikosi cha AFC Arusha. Nyoni aliwahi kucheza soka ya kulipwa Vital O ya Burundi kabla ya kutua Azam.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement