Shirikisho la soka la Ufaransa ‘FFF’ limethibitisha kurejea kambini kwa Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo Kylian Mbappe, baada ya kupatiwa matibabu ya pua hospitalini.

Mbappe alipata majeraha ya pua katika mchezo wa Mzunguuko wa kwanza wa Kundi D dhidi ya Austria jana usiku, baada ya kugongana na beki Kevin Danso dakika ya 90, hali iliyopelekea kushindwa kuendelea na mchezo.


Taarifa ya Shirikisho la Soka la Ufaransa imeeleza: “Mbappe amerejea kambini kujiunga na wachezaji wenzake akiwa katika hali nzuri, japo ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku kadhaa.”

“Matibabu ya Mbappe hayatahusisha upasuaji wa pua kama ilivyokuwa inadhaniwa hapo awali, kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji wetu akavaa ‘MASKI’ maalum ambayo itamsaidia atakapokuwa kwenye majukumu ya kuichezea timu ya Ufaransa wakati wa Michuano ya Euro 2024.”

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement