NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA NGUMU BONDIA YUSUF CHANGALAWE AMEPOTEZA PAMBANO LA KWANZA LA KUFUZU OLIMPIKI YA PARIS 2024
Bondia Mtanzania Yusuf Changalawe ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi amepoteza pambano lake la kwanza katika mashindano ya mwisho ya kufuzu kushiriki Olimpiki ya Paris 2024 kwa matokeo ya kutenganisha (split decision) ya points 3-2 dhidi ya mpinzani wake Cedrick Belony-Duliepre kutoka Haiti.
Pambano hilo lililofanyika katika Uwanja wa ndani wa Huamark, Bangkok - Thailand na kusimamiwa na mwamuzi Jung Sook CHO kutoka Korea Kusini, liliwashawishi majaji 3 dhidi ya 2 kumpatia ushindi Cedrick mkazi wa Montreal, Canada na kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Majaji 2 waliompa ushindi Changalawe ni kutoka Morocco 29:28 na Bulgaria 30:27 dhidi ya Argentina 30:27, Israel 29:28 na Sri Lanka 29:28 waliompa ushindi Cedrick.
Kwa matokeo hayo sasa yamemtoa Changalawe katika mashindano hayo ya kufuzu yanayoendelea nchini Thailand na sasa amebakiwa na tumaini moja tu katika nafasi 9 za usawa na upendeleo (Universality places)