NAHODHA WA TAIFA STARS MBWANA SAMATTA AMEIANDIKIA BARUA YA KUSTAAFU SOKA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF)
Nyota wa soka wa Afrika Mashariki Mbwana Samatta ameiandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuelezea nia yake ya kuacha kuichezea ‘Taifa Stars’.
Nyota huyo wa klabu ya PAOK inayoshiriki Ligi Kuu ya Ugiriki ambaye pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani, ni mmoja wa wana michezo walioiweka Tanzania kwenye ramani ya soka na kustaafu kwake huenda ikawa ni pigo kwa soka nchini humo.
Hata hivyo, TFF inasemekana kupinga ombi lake na kusisitiza kuwa bado inamtambua Samatta kama nahodha halali wa timu ya taifa ya Tanzania na kwamba wataketi chini na mchezaji huyo kumshawishi abadili wazo hilo.