MCHEZAJI na Nahodha wa klabu ya Simba, John Bocco ameiaga na kuishukuru klabu hiyo aliyoitumikia kwa mafanikio makubwa jambo linaloashiria mwisho wa utumishi wake klabuni hapo kama mchezaji.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii mfungaji huyo wa muda wote kwenye Ligi Kuu bara ameandika “First and last, Thank you Lion!”

Bocco kwa sasa yupo na timu ya Vijana ya wekundu hao wa Msimbazi ikiwa ni maandalizi ya maisha mapya ya ualimu wa kabumbu ndiye kinara wa mabao kwenye historia ya Ligi Kuu akipachika mabao 155.

Akiwa na umri wa miaka 34 John Bocco amecheza timu ya Taifa ya Tanzania michezo 74 na kufunga mabao 14 alianza kukitumikia kikosi cha Timu taifa mwaka 2009.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement