Baada ya siku ya jumapili kikosi cha FAR RABAT mabingwa watetezi wa kombe hilo la ligi maarufu kama BOTOLA kuweza kudondosha alama 2 kumeleta sura mpya kwenye msimamo wa ligi hiyo na sasa RAJA CASABLANCA wanaongoza ligi kwa points 1 yaani 69 kwa 68 za FAR RABAT 

Katika mchezo huo wa mzunguko wa 29 ambapo tumeshuhudia kikosi cha NASREDEN NABI kutoa sare dhidi ya MAT TETOUAN ambao walikua nyumbani na Mchezo huo ulitamatika kwa sare ya 2-2 na kuwapa nafasi RAJA CASABLANCA kuongoza ligi

NABII kocha ambae alianza vizuri na kuongoza ligi kwa muda mrefu mbele ya vigoo WYDAD CASABLANCA,RAJA CASABLANCA,RS BERKANE,FUS RABAT ameshindwa kutamba na kuruhusu kudondosha alama 2 

Kumbuka umebaki mchezo mmoja tu kukamilisha ligi hiyo ya BOTOLA ambapo maombi kubwa ni kwa FAR RABAT kushinda mchezo wa mwisho huku pia wakiomba RAJA CASABLANCA watoe sare au wafungwe.

Kocha NABI alitoka katika klabu ya Young Africa akiwa ametwaa mataji mawili ya ligi na FA lakini pia akiwa alifika fainali ya Caf Confederation Cup Je, NABI atachukua ubingwa msimu na klabu ya FAR RABAT kuendelea kutawala msimu wa pili mfululizo

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement