Mzunguko wa Tisa, Michuano ya NBC Championship umetamatika hapo jana kwa mchezo mmoja, Polisi Tanzania wakivuna Pointi tatu kwa ushindi wa Bao 2-0 mbele ya wageni wao Pan Africans FC katika Uwanja wa Ushirika, Mkoani Kilimanjaro.

Matokeo ya jumla mpaka kutamatika kwa mzunguko huo ni

 Mbeya Kwanza 2-1 Copco FC

 F.G.A Talents FC 1-1 Cosmopolitan FC

 Biashara United FC 2-1 Mbeya City FC

 Green Worriours FC 2-2 Mbuni FC

 Ruvu Shooting 1-3 Pamba Jiji FC

 Ken Gold FC 0-0 Stand United FC

 Transit Camp FC 0-1 TMA fc

 Polisi Tanzania FC 2-0 Pan Africans FC.


Kwa matokeo hayo, TMA anaongoza Ligi akiwa na Pointi 21 akimshusha Ken Gold ambaye anapointi 20 akishika nafasi ya Pili sambamba na Mbeya City anayeshika nafasi ya Tatu mwenye Pointi 20 tofauti ikiwa ni magoli ya kufunga na kufungwa huku Pamba jiji wakiwa nafasi ya Nne kwa kuwa na Pointi 18.

Ruvu Shooting wameendelea kuburuza mkia katika msimamo wa Ligi hiyo wenye jumla ya Timu shiriki 16 wakiwa na Pointi moja, Transit Camp wakiwa nafasi ya 15 wakiwa na Pointi tano kibindoni, Pan Africans FC wakiwa nafasi ya 14 kwa kuwa na pointi saba huku Cosmopolitan wakiwa na na Pointi Tisa wakiwa nafasi ya 13.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement