baada ya Stephane Aziz Ki kuwa nyota wa kwanza wa Yanga kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba, safari inaonekana ni zamu ya Clement Mzize kwani straika huyo amewaacha mbali viungo Khalid Aucho na Pacome Zouzoua katika mchuano mkali wa Novemba.

Aziz Ki, alinyakua tuzo ya Oktoba akiwabwaga beki mzawa, Dickson Job na kiungo Mkongo, Maxi Nzengeli, lakini safari hii Mzize ameonekana kuwakimbiza wenzake kwenye tuzo ya pili ya klabu hiyo. Licha ya Mzize kucheza dakika chache kwenye mechi

mbili za Ligi Kuu ndani ya Novemba dhidi ya Simba na Coastal Union akitumika kwa dakika 49 tu, lakini nyota huyo chipukizi amehusika mabao matatu kati ya sita waliyofunga.

Kwenye mechi ya watani akitokea benchi alitoa asisti mbili kwenye ushindi wa mabao 5-1, kisha akafunga bao pekee lililoizamisha Coastal kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Kwa upande wa Aucho ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi akitumika dakika 180 katika michezo miwili waliyocheza ndani ya mwezi huo.

Pacome ndiye anayefuata baada ya kucheza dakika 177 kwenye mechi dhidi ya Simba alicheza dakika 90 na kufunga bao moja kati ya matano waliyofunga na alicheza dakika 87 dhidi ya Coastal Union. Akizungumza, Mzize alisema kitendo cha kutajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo hiyo kwake ni ushindi mkubwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement