Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin na mshambuliaji wa timu hiyo, Kibu Denis wametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kila mmoja kwa kosa la kuonekana wakiondoa taulo la kipa wa Coastal Union, Ley Matampi alilokuwa ameliweka pembeni mwa lango kitendo kilichotafsiriwa kuashiria imani za kishirikina wakati wa mchezo wa Ligi Kuu wa timu hizo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Machi 9, 2024.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 41:5 ya Ligi Kuu kuhusu udhubiti wa klabu.

Kwenye mchezo huo Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-1.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement