Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji "MO" amefanya kikao na Viongozi mbalimbali wa klabu hiyo ili kufahamu changamoto za klabu hiyo zipo wapi na namna ya kuzitatua.


Kupitia kurasa zake mitandao ya kijamii MO ameandika “Nimefanya kikao na Viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua, kikao kimeenda vizuri, WanaSimba tusife moyo, tuendele kushirikiana nguvu moja"

Baadhi ya Viongozi walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi Simba Salim Abdallah Muhene (Try Again), Mwenyekiti wa zamani Simba SC Swedi Nkwabi na Mshauri wa Mo Dewji Crescentuis Magori.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement