Mwamuzi wa kati wa mchezo kati ya Coastal Union na Yanga Sc, Emmanuel Mwandembwa amefungiwa miezi sita (6) kufanya kazi ya uamuzi wa mpira wa miguu, kwa kosa la kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za mpira wa miguu jambo lililosababisha ashindwe kumudu mchezo husika.

Aidha Kamati ya Undeshaji na Usimamizi wa Ligi imefuta kadi ya njano aliyoonyeshwa mchezaji Semfuko Charles wa Coastal Union baada ya kujiridhisha kuwa mchezaji huyo hakustahili adhabu hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement