Mwanariadha wa masafa marefu kutoka nchini Morocco Fatima Ezzahra Gardadi anakuwa atashiriki kwa mara ya kwanza Olimpiki 2024 Paris nchini Ufaransa lakini hilo halijakatisha tamaa yake.



Gardadi mwenye umri wa miaka 32 alikua mwanariadha wa mbio za marathon pekee mwaka wa 2019. Miaka minne baadaye mnamo 2023, alifuzu kwa Olimpiki yake ya kwanza baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye Mashindano ya Riadha ya Dunia huko Budapest.

Kabla ya kubadili mbio za marathon, alikuwa ameshiriki mbio za mita 800, 1,500, 3,000, 5,000, 10,000 na nusu marathon bila mafanikio mengi. 

Maandalizi yake ya Olimpiki yalianza vizuri alipomaliza wa pili katika mbio za Xiamen marathon nchini China mnamo Januari baada ya kutumia saa 2:24:12.


Bekelech Gudeta Borecha wa Ethiopia ndiye aliyebeba siku hiyo. Alimaliza kwa 2:22:54.

Mwanariadha huyo anafanya mazoezi huko Marrakech, chini ya usimamizi wa mumewe, mwanariadha Mustapha El Houdadi.

Medali yake ya shaba huko Budapest ilimfanya kuwa mwanamke wa kwanza wa Morocco kushinda medali ya marathon katika michuano ya Dunia.

"Matarajio yangu ni kushinda medali katika Olimpiki na kuwakilisha Morocco vyema wakati wa Michezo hii,"Alisema Fatima.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement