Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon za wanaume, Kelvin Kiptum, anatarajiwa kuzikwa baadaye Ijumaa nyumbani kwake Eldoret magharibi mwa Kenya.

Rais wa Kenya William Ruto ataongoza waombolezaji katika kumuenzi mwanariadha mahiri ambaye aliweka na kuvunja rekodi katika maisha yake mafupi ya mbio.



Kiptum alifariki katika ajali ya gari, akiwa na umri wa miaka 24 pekee, wiki mbili zilizopita.

Maelfu wametoa heshima kwa Kiptum katika mji wake wa asili.

Umati wa watu ulikusanyika njiani mjini Eldoret huku gari la maiti likiendeshwa hadi kijijini kwake kabla ya mazishi.



Kazi yake kama mwanariadha ilikuwa inaanza tu.

Katika miaka miwili, angekimbia marathoni tatu kati ya saba za kasi zaidi katika historia, akavunja rekodi ya dunia na kuweka rekodi ya mbio za London.

Alikuwa amejiwekea malengo ya kukimbia mbio fupi za saa mbili za marathon huko Rotterdam mwezi huu wa Aprili.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement