Nyota wa riadha wa Somalia, Abdullahi Jama aliweka historia kwa kuwa mwanariadha wa kwanza wa nchi hiyo kutwaa medali kwenye mashindano ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 35.

Jama alishinda medali ya fedha baada ya kumaliza wa pili katika mbio za mita 5000 kwenye mashindano ya michezo ya Afrika iliyoandaliwa katika uwanja wa spoti wa chuo kikuu cha Ghana, Accra mnamo mwezi Machi.

Jama alitumia muda wa 13:38.64 na kupata medali ya fedha.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh ametoa heshima ya juu zaidi ya kitaifa katika michezo kwa mwanariadha huyo.




You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement