MWAKINYO AFUNGIWA NGUMI MWAKA MMOJA
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania imetangaza kumfungia bondia raia wa Tanzania Hassan Mwakinyo kutopanda ulingoni kupigana kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano ambalo liliandaliwa na kampuni ya PAF Promotion.
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania pia imempiga faini Bondia Hassan Mwakinyo ya Milioni Moja.
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania imethibitisha kuwa adhabu hiyo haizuii PAF Promotion kwenda mahakamani.