Mtu mmoja amefariki Dunia na wengine Watatu kujeruhiwa baada ya gari aina ya Toyota Coaster iliyobeba mashabiki kadhaa wa Timu ya Simba kutoka Mbeya kupata ajali ya kugongana na Lori maeneo ya Vigwaza Mkoani Pwani, Alfajiri ya leo Machi 29, 2024

Taarifa ya kifo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo ambaye amesema “Nipo eneo la tukio tunaendelea kutoa magari. Chanzo cha ajali na taarifa nyingine zinaendelea kuchunguzwa na zitatolewa baadaye.”

Mashabiki hao walikuwa njiani kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa timu yao dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye Uwanja wa Mkapa ikiwa ni Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa usiku wa leo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement