Kamati ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), inayosimamia soka la vijana imeipokonya Mtibwa Sugar (U20) pointi 15 kwa kosa la kutofika kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliopangwa kuchezwa Machi 19, 2024, kwenye Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na shirikisho hilo, imesema kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kujiridhisha timu hiyo haikuwa na sababu za msingi kushindwa kufika kwenye mchezo husika.

Uamuzi huo umefikiwa na kamati kwa kuzingatia Kanuni ya 31.1.3 ya Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2023.

Aidha kamati hiyo imeipa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu timu ya JKT Tanzania kwa mujibu wa kanuni ya 17:44 wa Kanuni za Ligi Kuu toleo la 2023.

Mtibwa iliyopo kwenye kundi B sasa itaporomoka kutoka nafasi ya pili hadi nafasi ya saba katika timu nane, ikiwa na pointi nane juu ya Tabora United inayoshika mkia na pointi sita.

JKT Tanzania itapanda kutoka nafasi ya sita hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 21, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Dodoma Jiji yenye pointi 28.

Hata hivyo, kundi hilo lenye timu nane, timu zote zimecheza mechi 13 na kubakiza mechi moja pekee







You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement