Katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa na miundombuni bora ya kimichezo, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imemtaka mkandarasi anayesimamia ujenzi wa viwanja na eneo la kupumzikia katika eneo la Changamani, jijini dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ameyasema hayo alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi huo ambapo amemtaka mkandarasi huyo kuhakikisha ujenzi huo unakamilika Mwezi Machi mwakani.

“Sasa nimekuja hapa nimekuta kazi imefika asilimia takribani 29 na 30, tupo nyuma kwa miezi miwili, nimemuelekeza mkandarasi kuhakikisha kazi wanafanya haraka, ” Gerson Msigwa.

Msigwa ameeleza kuwa, kwa kiwango kilichofikia ujenzi huo, ni changamoto kutokana na kazi hiyo kuwa katika awamu tatu huku akiweka wazi juu ya mipango waliyojiwekea juu ya kukamilika kwa ujenzi huo.

“Sasa tunachangamoto hapa kwasababu tupo nyuma kwa takribani miezi miwili, na mradi huu unaawamu tatu ambapo awamu ya kwanza inatakiwa iwe imekamilika mweiz machi mwaka 2024, awamu ya pili inatakiwa ikamilike miezi sita baadaye na awamu ya tatu inatakiwa tena ikamilike miezi sita baadaye, kwahiyo kazi kubwa inatakiwa ifanyike hapa, na nimemtaka mkandarasi wahakikishe wanaongeza kasi ya ujenzi, ” Gerson Msigwa 

Msigwa ameeleza kuwa, Dar es salaam nan chi ya Tanzania kwa ujumla kunamahitaji makubwa sana ya maeneo ya kufanyia mazoezi, kucheza na kupumzikia hivyo serikali imeanza kwa Dar es salaam na Dodoma huku wakiwa na mipango ya kwenda mikoa mingine.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement