Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford ameripotiwa kuweka wazi mipango yake baada ya kuhusishwa kuwa anataka kuondoka timu hiyo.

Rashford ambaye hakufanya vizuri msimu uliopita akicheza mechi 43 za mashindano yote na kufunga mabao manane tu huku akiandamwa na kesi nyingi za utovu wa nidhamu nje ya uwanja, alikuwa akihusishwa kuondoka katika dirisha hili ili kujiunga na PSG ili akawe mbadala wa Kylian Mbappe.

Hata hivyo, Rashford anadaiwa kutaka kusalia Old Trafford kwa msimu ujao na amezungumza na kocha wa timu hiyo Erik ten Hag, akimwambia kwamba atabadilika na kuwa bora zaidi.

Kwa mujibu wa The Sun, Chanzo cha karibu na staa huyu kimesema, Ten Hag amemwambia Rashford kwamba bado yupo katika mipango yake.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement