Yanga Imepata wakati mgumu kimataifa msimu huu baada ya kukosa mshambuliaji wa uhakika kutoka na Hafidhi Konkoni, Kennedy Musonda na Clement Mzize kushindwa kumshawishi kocha Miguel Gamondi, sasa ni rasmi kuwa kocha huyo atasajili mshambuliaji kwenye dirisha hili. Ranga Chivaviro wa Kaizer Chief anatajwa kumalizana na Yanga. Timu hiyo itahaha kumpata mshambuliaji mkubwa kutoka kwenye timu nyingine ambazo hazijashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwa kuwa kanuni haimruhusu mchezaji kuzichezea timu mbili kwenye michuano hiyo, endapo tu itakuwa na uhakika wa kwenda robo fainali.

Hivyo wakati usajili unafunguliwa Desemba 16, tayari Yanga itakuwa imeshavaana na Medeama Desemba 8, mchezo huu utaipa picha halisi ya kama ina nafasi ya kusonga mbele au hapana. Endapo Yanga itashinda mchezo huu, itafikisha pointi nne na kubakiza michezo mitatu ambayo ina pointi 9, lakini miwili kati ya hiyo itakuwa nyumbani. Hivyo ili Yanga isajili mshambuliaji mkubwa inatakiwa kushinda mchezo huu hali ambayo itamfanya kocha wa timu hiyo atafute staa ambaye anaweza kuwavusha kwenye michezo mitatu inayofuata, dhidi ya Medeanma Desemba 20, Belaouzdad Februari 23 pamoja na ule dhidi ya Al Ahly Machi 1.

Hata hivyo, hali inaweza kuwa tofauti kwa Yanga, endapo watapoteza mchezo dhidi ya Medeama kwa kuwa matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali yatafifia, hivyo timu hiyo itapunguza kasi ya mshambuliaji mkubwa ikiamini kuwa inaweza kumpata yule aliye bora zaidi kwenye dirisha kubwa la Julai na waliopo wanaweza kusaidia kwenye ligi. Hii ni kwa kuwa wachezaji wengi wakubwa huwa sokoni kwenye dirisha kubwa kuliko dirisha dogo ambalo timu nyingi huwa kwenye mipango nao na hata bei za mastaa hao huwa juu.

Mbali na eneo hilo, Yanga inalazimika pia kumsajili beki mmoja wa kati baada ya Gift Fred ambaye alisajiliwa kwenye kipindi kilichopita kushindwa kuonyesha makali yake, huku pia ikionekana inaweza kuongeza kiungo mkabaji atakayesaidiana na Khalid Aucho ambaye amekosa mbadala sahihi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement