Msako wa Parimatch Bingwa Season 3 unaendelea kufanya Audition zake Mikoani ambapo baada ya Arusha kufanya vizuri Msako umefika mpaka makao makuu ya Nchi na vijana wamejitokeza kwa wingi. 


Bingwa imefanyika kwa siku mbili Royal Village May 25 na 26 na kukutana na vijana wengi zaidi ambao wamejitokeza kuonyesha vipaji vyao ili kupata bahati ya kuingia kwenye jumba la Bingwa Dar es salaam, baada ya kupita kwenye mchujo wa Majaji watatu ambao kwa Dodoma walikuwa ni Jimmy Jamal, Ndaro pamoja na Chief Jaji Aaliyah. 


Mchakato huu wa kuwasaka washiriki wa Parimatch Bingwa msimu wa Tatu utaendelea Mwanza wikiendi ijayo baadae utaenda Mbeya na kumaliza na Dar Es Salaam kabla ya Washiriki kuingia kwenye jumba la Bingwa kwa siku 70


Kwa namna ambavyo mchakato unaenda mpaka sasa unahisi mshindi wa Bingwa atakakuwa anatoka mkoa gani?


Fuatilia mchakato huu mzima kupitia TV3 kwenye kisumbuzi cha Startimes na updates zote zitakuwa zinawekwa kwenye kurasa za TV3 Instagram, Bingwa Show Instagram pamoja na ukurasa wa Parimatch

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement