Katika kuendelea kukuza michezo ikiwa ni sambamba na kuboresha Miundombinu ya Kimichezo nchini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeweka wazi juu ya ujenzi wa kituo cha Michezo cha Mlya kilichopo Jijini Mwanza.

Akijibu hoja ya Mbunge wa Sumve, Kasalali Mageni aliyehoji kwanini wizara inahamisha ujenzi wa Kituo cha Michezo Malya kutoka Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza kwenda Ilemela wakati imeshasaini Mkataba wa utekelezaji Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt: Damas Ndumbaro ameeleza kuwa hawajahamisha eneo la ujenzi wa uwanja huo, lakini wanaendelea na ujenzi wa kituo cha michezo katika Wilaya ya Ilelema.

"Tutaendelea na ujenzi wa Kituo Cha Michezo Malya kama ambavyo tumepanga, hatujahamisha ujenzi huo kwenda sehemu nyingine, lakini pia tutaendelea na ujenzi wa Kituo cha Michezo katika Wilaya ya Ilemela na maeneo mengine, kwa kuwa azma ya Serikali ni kuwa na vituo pamoja na akademia za michezo katika maeneo mbalimbali nchini, " Waziri Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro ameongeza kuwa, Baada ya Wizara kusaini mkataba wa ujenzi huo, bado hawajaenda Saiti kwasababu wanafanya Uhamasishaji wa Fedha huku akiahidi utekelezaji wa ujenzi huo kuendelea.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement