Mo alikutana na wachezaji vyumbani kwenye Dimba la Mkapa na kuwawekea kitita cha shilingi milioni 500 mezani kama watafanikiwa kushinda dhidi ya Al Ahly.

Mo alitoa ahadi yake mapema tu kabla ya mchezo wa kwanza pale kwa Mkapa ambapo aliwaambia wachezaji kama watashinda mchezo huo, basi atawapa shilingi milioni 500 ikiwa ni sehemu ya hamasa yake, huku akiwaambia zile posho za siku zote zitabaki kama kawaida, hivyo kama tukishinda katika mchezo wa marudiano, kuna zaidi ya shilingi milioni 500 wachezaji watapata.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement