Taarifa hiyo imetolewa leo, Septemba 4, 2025, kwa wanachama, wapenzi na wadau wa Simba SC, ambapo Mo Dewji ameeleza kuwa ameamua kuachia nafasi hiyo kutokana na majukumu mengine pamoja na ukweli kwamba mara nyingi yupo mbali na shughuli za kila siku za klabu.

“Nitaendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Simba SC, lakini nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi sasa inakabidhiwa kwa kiongozi mpya mwenye muda na ukaribu zaidi,” alisema Mo Dewji.


Kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Kampuni (MEMARTS) ya Simba Sports Club Company Limited, Rais anatokana na MO Simba Company Ltd na anayo mamlaka ya kuteua viongozi wa Bodi.

Mbali na kumteua Magori, Mo Dewji pia ametangaza majina ya wajumbe wapya wa Bodi upande wa Mwekezaji, ambao ni:

  • Barbara Gonzalez
  • Hussein Kitta
  • Azim Dewji
  • Rashid Shangazi
  • Swedi Mkwabi
  • Zuly Chandoo
  • George Ruhango

Mo Dewji amewashukuru viongozi wote waliowahi kushika nafasi za uongozi ndani ya Simba SC kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo, huku akisisitiza kuwa timu mpya ya uongozi italeta msukumo mpya kuelekea ndoto ya Simba SC ya kuwa klabu bora barani Afrika.

“Nina imani timu hii mpya ya uongozi itaendeleza ndoto ya Simba SC ya kuwa klabu bora barani Afrika,” ameongeza.


You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement