Timu ya JKT Tanzania imetozwa faini ya Sh 1 milioni na kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Tanzania kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mchezo baina yao na Mashujaa uliopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Taarifa ya Bodi ya Ligi imeeleza kuwa wachezaji wa JKT walitumia mlango wa VIP badala ya mlango rasmi kama walivyo elekezwa kwenye kikao cha kitaalam cha maandalizi ya mchezo.

Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 17:21 na 17:60 ya ligi kuu kuhusu taratibu za mchezo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement