“Sio kweli.” Mke wa zamani wa Kaka akanusha uvumi kwamba alitalikiana na mchezaji huyo kwa sababu alikuwa ‘mkamilifu sana’.

Mke wa zamani wa mchezaji wa kimataifa wa Brazil na nyota wa zamani wa AC Milan na Real Madrid, Ricardo Kaka, Caroline Celico, amekanusha uvumi uliotapakaa kuhusu kuachana kwao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Celico alisema.

“Kwa bahati mbaya tunasikia habari za uongo na nukuu FEKI. Ngoja nikusahihishe. Nilitalikiana karibu miaka 10 iliyopita hata hivyo nilipata watoto wawili wa kupendeza ndani ya miaka hiyo 14 ya uhusiano’'.

Celico alisisitiza kwamba kuachana kwao kulitokana na makubaliano yao wawili, licha ya uvumi kwamba alimwacha Kaka kwa sababu alikuwa mkamilifu sana.

“Imekuwa karibu miaka 8. Niko na mume wangu Eduardo, na tutapata mtoto wetu wa kwanza mwezi ujao Ninaheshimu sana simulizi ya maisha yangu, na ninashukuru sana kwa kila kitu ambacho nimeishi hadi sasa. Mume wangu wa zamani na mimi tulipitia njia nzuri ya kulea watoto wetu, na ninashukuru sana kwa hili’, Aliongeza.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement