MKATABA WA MASHARTI YA KIPEKEE ALIYOINGIA KINDA WA TIMU YA TAIFA YA BRAZIL PRODIGY ENDRICK NA MPENZI WAKE
Prodigy Endrick ambaye ni mchezaji chipukizi wa Brazil, akiwa na umri wa miaka 17, ameshika vichwa vya habari baada ya kuweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake aitwaye Gabriely Miranda, mwenye umri wa miaka 21, wameandikiana mkataba wa mahusiano yao, ambao umeonekana kuwa na masharti ya kipekee.
Endrick ameyasema hayo akiwa na mpenzi wake katika mahojiano katika Podcast ya "Pod Delas" ambapo miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na:
1. Marufuku kuonyesha mabadiliko makubwa ya kitabia pamoja na uraibu, pia ni lazima kusema neno "Nakupenda" katika hali zote.
2. Pande zote mbili 'haziruhusiwi kubishana' katika maeneo ya umma.
3. Pande zote mbili haziruhisiwi kuwa na uhusiano wa kimapenzi au wa karibu na watu wengine, wakiwemo wapenzi wao wa zamani.
4. Endapo mmojawapo atakiuka masharti hayo atalazimika kutoa faini kwa njia ya zawadi.