Mkataba wa kitambaa cha kunawa mkono wa kwanza wa Lionel Messi na Barcelona wakati huo akiwa na umri wa miaka 13 kupigwa mnada kwa bei ya kuanzia £300,000.

Mkataba huo ulisainiwa Desemba 2000, una ahadi kutoka kwa mkurugenzi wa wakati huo wa Barca Carles Rexach kumsajili Messi.

Pia ulisainiwa na Josep Minguella, mshauri wa uhamisho wa klabu ya Uhispania, na wakala Horacio Gaggioli, ambaye alipendekeza Muargentina huyo.

Messi alijiunga na Barca mwezi mmoja baadaye na kuwa mfungaji bora wao.

Alianza kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na kufunga mabao 672 katika michezo 778 kwenye klabu hiyo ya Catalan.

Sasa akiwa na umri wa miaka 36, ​​Messi ameshinda mataji 10 ya La Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa akiwa Barcelona kabla ya kuondoka kwenda Paris St-Germain mnamo mwaka 2021.

Mkataba huo ulitiwa saini katika mkutano uliopangwa na Rexach, ambaye alimwalika babake Messi Jorge kwenye chakula cha mchana baada ya wasiwasi kutoka kwa familia ya Messi kuhusu ukimya wa Barcelona kufuatia majaribio ya awali ya kijana huyo.

Kwa wino wa bluu, makubaliano kwenye mkataba huo wa kitambaa yanasomeka: "Huko Barcelona, ​​tarehe 14 Desemba 2000 na uwepo wa Messrs Minguella na Horacio, Carles Rexach, mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona,​​anakubali, chini ya wajibu wake na bila maoni yoyote ya kupinga, kumsajili mchezaji Lionel Messi, ili mradi tu tuzingatie kiasi cha pesa kilichokubaliwa."

Mkataba huo utauzwa kupitia nyumba ya mnada ya Uingereza Bonhams mwezi Machi.

Mkuu wa vitabu bora na maandishi huko Bonhams Ian Ehling alisema: "Hii ni mojawapo ya vitu vya kusisimua zaidi ambavyo nimewahi kushughulikia.

"Ndio, ni kitambaa kilicho kama karatasi, lakini ni kitambaa maarufu kilichokuwepo wakati wa mwanzo wa taaluma ya Lionel Messi.

"Kilibadilisha maisha ya Messi, mustakabali wa FC Barcelona, ​​na kilikuwa muhimu kuwezesha utoaji wa baadhi ya nyakati bora za soka kwa mabilioni ya mashabiki duniani kote."












You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement