Congo DR ambao wamewahi kuchukua kombe la AFCON mara mbili, leo wamefanikiwa kuingia robo fainali ya AFCON 2023 kwa kuitoa Egypt kwenye penati 8-7.

Wakati Egypt wakiwa ni Mabingwa wa kihistoria wa AFCON wakilibeba kombe hilo mara 7 ambazo ni mara nyingi kuliko Taifa lolote, Congo wao wamewahi kulibeba mara mbili ambapo mara ya kwanza ilikua ni 1968 wakiitwa Congo Kinshasa na mara ya pili mwaka 1974 wakiitwa Zaire.

Kituo kinachofuata na Congo DR uso kwa uso na Guinea.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement