Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali, inatarajiwa kuanza kuchezwa leo Jumanne ambapo kutakuwa na mechi mbili saa 4:00 usiku, ambazo ni Arsenal dhidi ya Bayern Munich itapigwa Uwanja wa Emirates, huku Real Madrid ikiwa mwenyeji wa Manchester City kunako Dimba la Santiago Bernabeu.

mchezo ambao wengi wanasubiri kuona kama Arsenal italipa kisasi kwa Bayern baada ya kunyanyaswa mechi mbili za mwisho walizokutana kwenye michuano hiyo msimu wa 2016/17, ambapo ndiyo Arsenal ilikuwa mwisho kushiriki kabla ya kurejea tena msimu huu.

Matokeo ya jumla ya mabao 10-2 waliyopata Bayern dhidi ya Arsenal, ndiyo yanazungumzwa zaidi kipindi hiki kuelekea mchezo wa leo ambapo Arsenal inaonekana kuwa vizuri zaidi ya Bayern. Je, italipa kisasi au rekodi itawabeba Bayern?

Huu ni mchezo unaowakutanisha mabingwa watetezi, Man City dhidi ya mabingwa wa kihistoria, Real Madrid.

Rekodi zinaonesha kwamba, timu hizo zimekutana mara 10 katika michuano hii, Man City inaongoza kwa kushinda mechi nyingi (4) na kufunga mabao 17, huku ikibeba taji moja msimu uliopita lililokuwa likishikiliwa na Madrid.

Kwa upande wa Madrid, imeshinda mechi 3, imefunga mabao 14, ikishinda mataji 14 na ndiyo timu yenye mataji mengi ndani ya michuano hiyo.

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana katika mchezo wa nusu fainali msimu uliopita, Man City ikashinda kwa jumla ya mabao 5-1, baada ya mchezo wa kwanza pale Bernabeu kumalizika kwa sare ya 1-1, kule Etihad, Man City ikashinda 4-0. Ikaenda fainali kubeba kombe lao la kwanza la michuano hiyo.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement