KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta ameweka wazi kuwa anaamini na amejipanga kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wake.

Arteta amesema kuwa Chelsea walio nafasi ya tisa watakuwa wapinzani hatari bila kujali kama Palmer yuko fiti.

Arteta amesema kuwa nafasi waliyopo haimaanishi Chelsea hawapo vizuri bali wanakikosi chanye ubora mzuri zaidi ya wengi wanavyodhani na kuweka wazi kuwa wanastahili kuwa katika nafasi ya juu zaidi kwenye ligi ukiangalia wamefanya nini na wamezalisha nini kwenye michezo.

Kwa upande wa Kocha mkuu wa Chelsea Mauricio Pochettino amesisitiza kwamba hana wasiwasi wowote kuhusu hali ya kikosi chakekuelekea mchezo dhidi ya Arsenal.

Ikumbukwe kuwa Jumamosi jioni, The Blues walikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Manchester City kwenye nusu fainali ya Kombe la FA.

Kikosi cha Pochettino sasa kimesalia kujaribu kupata kufuzu kwa Uropa kupitia Ligi hiyo ambayo wanashika nafasi ya Tisa katika msimamo.

Chelsea wameshinda mechi moja tu kati ya tisa zilizopita dhidi ya Arsenal, hiyo ikiwa ni bao 2-0 huko Emirates mnamo Agosti 2021 wakati Romelu Lukaku alipocheza kwa mara ya pili katika klabu hiyo.

Hata hivyo, Chelsea wamepoteza mechi sita kati ya nane katika kipindi hicho, ikiwa ni pamoja na mechi tatu mfululizo kwa nyakati mbili tofauti, huku pia wakiwa mbele kwa mabao mawili katika mechi ya marudiano ya msimu huu kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kutoka sare ya bao 2-2. .

Pochettino ameweka wazi kuwa angependelea kuona orodha ya wachezaji majeruhi ikipunguza kabla ya mchezo wa hii leo lakini anauwezekano wa kuwakosa achezaji watatu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement