MICHUANO YA EURO 2024 YALETA MABADILIKO KATIKA UWASILISHAJI WA UAMUZI VIWANJANI
Kidogo kuna mabadiliko katika michuano hii kwenye masuala ya uamuzi, kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ya Shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya (UEFA), Roberto Rosetti ni kwamba, makapteni wa timu pekee ndio wanaruhusiwa kuzungumza na mwamuzi wakati wa mechi na si vinginevyo.
Vilevile ikitokea timu kapteni wao ni golikipa kama ilivyo kwa Italia (Gianluigi Donnarumma) na Slovenia (Jan Oblak), benchi la ufundi la timu hizi litatakiwa kumtaarifu mwamuzi kwamba ni mchezaji gani wa ndani ambaye atakuwa akiwasiliana naye wakati wa mechi, kwa sababu itakuwa ngumu kwa mwamuzi kwenda na kurudi kuzungumza na kipa.
Mbali ya hili, pia kutakuwa na utaratibu wa mwamuzi kuelezea mashabiki juu ya uamuzi alioufanya baada ya kwenda kwenye VAR.