Michuano ya CECAFA Dar Port Kagame Cup kuendelea kutimua vumbi hii leo kwa mechi za mwisho hatua ya makundi kupigwa dimba la Chamazi Complex sambamba na KMC.

Mkurugenzi Mtendaji wa CECAFA Auka Gecheo amezungumzia mwenendo wa mashindano hayo na kuweka wazi juu ya Kiwango cha ushindani kiwa juu ikizingatiwa washiriki wengi ni mabingwa wa kujitegemea kutoka ligi za nchi husika.

SC Villa kuvaana na APR FC, Singida Black Stars dhidi ya El Merriekh, JKU dhidi ya Dekadaha na Coastal Union dhidi ya Al Wadi FC.

Mpaka sasa kunako msimamo hatua ya makundi Kundi A linaongozwa na Al Wadi FC wakiwa na alama sita wakifuatiwa na JKU wenye alama tatu, Coastal Union alama Tatu pia huku Dekedaha wakiwa hawana alama.

Kundi B Ni Al Hilal wakiongoza kundi wakiwa na Alama sita, Red Arrows alama Tatu, Gor mahia alama moja wakifungana na Djibout Telecom huku Kundi C APR wakiwa na alama sita, SC Villa alama nne, El Merreikh alama moja na Singida Black Stars wakiwa hawajaambulia alama yoyote.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement