πŸ‡ΈπŸ‡³ - πŸ‡¬πŸ‡² Senegal - Gambia πŸ…² 5pm* 

Mabingwa watetezi Senegal kuanza safari ya kulihifadhi taji lao, mechi za kundi C nao wenyeji wa Kombe la Afcon lililopita, Cameroon, wakishuka dimbani ikiwa ni siku ya tatu ya Kombe la Afcon linaloendelea nchini CΓ΄te d’Ivoire.

Senegal itakutana na Gambia inayoshiriki Afcon kwa mara yake ya pili huku Sadio Mane, aliyeuasi ukapera hivi karibuni, akisalia kuwa tumaini la Simba wa Teranga.


πŸ‡¨πŸ‡² - πŸ‡¬πŸ‡³ Cameroon - Guinea πŸ…² 8pm 

Aidha, Cameroon, inayoongozwa na Rigobert Song, itakuwa inamtegemea Vincent Aboubakar itakapakwaruzana na Guinea, iliyojihami na mfungaji hatari Serhou Guirassy, anayeichezea Stuttgart ya Ujerumani.


πŸ‡©πŸ‡Ώ - πŸ‡¦πŸ‡΄ Algeria - Angola πŸ…³ 11pm

Mbali na Kundi C, Riyad Mahrez naye atakuwa uwanjani Stade de la Paix Bouake, mbweha wa jangwani wakitoana jasho na Angola mechi ya Kundi D.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement