Michezo ni sekta muhimu katika dunia ya Sasa. Michezo hutoa ajira, huingiza kipato, huliingizia Taifa kodi za kutosha, hujenga afya ya jamii, hujenga uhusiano katika Jamii, husaidia ukuaji kielimu kwa watoto na vijana na Michezo ni nyenzo muhimu katika diplomasia ya Kimataifa kote duniani.

Sekta ya Michezo inatajwa kuwa sekta ya kiuchumi inayokuwa kwa kasi sana duniani. Kwa nchi ya Marekani ripoti zinaonesha kuwa nchi hiyo huingiza takribani Dola bilioni 15 kwa mwaka kama pato la moja kwa moja kwa watu takribani laki tano walioajiriwa katika sekta hiyo.

Huu ndio Utalii wa michezo anaopambana kuukuza mkoani Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda. Kupitia Michezo anaamini kuwa Ataioanisha na Utalii wa hifadhini na hivyo kusaidia kukuza pato la mtu mmoja mmoja na Pato la Arusha kwa ujumla kupitia Michezo na watalii ambao hufika Arusha kwa mambo mbalimbali.

Kama Ilivyo Rwanda, Mkuu wa Mkoa pia anavutia uwekezaji katika sekta ya Utalii wa mikutano ya kimataifa.Rwanda kwa mwaka 2023 kupitia Ofisi ya Mikutano na Matukio (MICE) ilirekodi mapato ya Dola milioni 95 kupitia mikutano.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Makonda anaamini kupitia mikutano, michezo na Utalii bhasi ipo namna kila mmoja anaweza kunufaika kuanzia kwa wajasiriamali wadogo ikiwemo wauza mbogamboga, wasafirishaji, mpaka kwa wenye mahoteli na sehemu za kulala wageni.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement