Meja mstaafu Michael Changarawe ambaye pia ni Bondia mstaafu ametaka dira mpya ya maendeleo ya mwaka 2050 izingatie zaidi ukuzaji wa vipaji kwa kutumia mazingira halisi yaliyopo nchini Tanzania.

Akichangia maoni yake kwenye dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, Meja mstaafu Changarawe ameshangazwa na serikali kufuta michezo mingi mashuleni akitaka uwekezaji zaidi kwenye ukuzaji wa vipaji kwa watoto ili kuondokana na tatizo la ajira lililopo duniani kote.

Ameitaka serikali kuwekeza kikanda katika kufundisha michezo mbalimbali, akitolea mfano Kanda ya ziwa na uwepo wa ziwa Viktoria na kutaka watoto wa Kanda ya ziwa kufundishwa kuhusu Michezo ya kuogelea, ndondi pamoja na michezo mingine kulingana na mazingira ya kanda ya ziwa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement