Michezo ya mwisho ya Ligi itapigwa mwishoni mwa wiki hii ikizikutanisha Mbuni FC wakiwa nyumbani Dimba la Sheikh Amri Abeid, Arusha kumkaribisha Pamba FC, TMA dhidi ya Copco Dimba la Black Rhino jijini Arusha, Biashara United dhidi ya Cosmo Politan Dimba la Karume Mkoani Mara, Pan African dhidi ya Stand United Dimba la Jenerali Isamuhyo na FGA Talents dhidi ya Mbeya City Dimba la Majimaji Mkoani Ruvuma.

Michezo mingine ni Kengold ambao wameshapanda daraja kushiriki Ligi kuu msimu ujao wakivaana na Polisi Tanzania Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Green Worriors dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini Mkoani pwani na Uwanja wa Nang’wanda Sijaona Mkoani Mtwara ukishuhudia mwenyeji Mbeya Kwanza akimkaribisha Transit Camp.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement