Safari ya Barcelona kwenda Paris St-Germain ilikuwa ya kufana kwani washindi mara tano walitoka nyuma na kupata ushindi wa 3-2 kabla ya mkondo wa pili Jumanne ijayo.

Winga wa zamani wa Leeds, Raphinha aling'ara jijini Paris, huku Kylian Mbappe akishindwa kutamba.

Pia kulikuwa na baadhi ya vijana waliovunja rekodi katika upande wa Barcelona, ambao walionyesha mchezomzuri mbele ya umati wa watu wa Parisi wenye chuki walipokuwa wakiwafuata.



Winga wa Brazil Raphinha hakuwahi kufunga katika Ligi ya Mabingwa kabla ya mechi ya Jumatano mjini Paris, lakini usingejua kuhusu ubora wake karibu na lango.

Kwa bao lake la kwanza, alitumia makosa ya Gianluigi Donnarumma .

Bao lake la pili, ambalo lilifanya Barcelona kusawazisha , lilionyesha ustadi wa hali ya juu alipotazama pasi iliyokatwa ya Pedri ikija begani mwake kabla ya kulifunga kwamguu wake wa kushoto.










You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement