Nusu Fainali ya Kombe la FA kutimua vumbi hapo kesho kwa Manchester City kukutana na Chelsea huku Coventry dhidi ya Manchester United huku ikielezwa kuwa Chelsea na Man City huenda zikakosa wachezaji 11 muhimu katika mchezo wao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Wembley

Kwa upande wa Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa huenda ikaendelea kumkosa Beki wake Levi Colwill kutokana na kuwa na jeraha la vidole.

Colwill amekosa mechi sita zilizopita za Chelsea kutokana na tatizo hilo ambalo hatimaye liligunduliwa kwa mara ya kwanza dhidi ya Crystal Palace mwezi Februari.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, ambaye alilazimika kuvaa kiatu cha kujikinga kama sehemu yamatibabu, alianza mazoezi mepesi wiki chache zilizopita huku akitazamiwa kucheza mechi dhidi ya vijana wa Pep Guardiola kwenye Uwanja wa Wembley.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement