Nyota wa zamani wa Simba wameipa ramani timu hiyo ya kuibuka na ushindi kesho katika mchezo wa tatu wwa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika wakati itakapokuwa wageni wa Wydad Casablanca ya Morocco katika mechi itakayopigwa Marrakesh.

nyota wa zamani wa kikosi hicho wameitaka timu hiyo kucheza kwa tahadhari kubwa. Mtemi Ramadhan alisema licha ya matokeo mabovu ya Wydad katika michezo yao miwili ya hatua ya makundi iliyopita ila haitokuwa mechi nyepesi kwa Simba hivyo wanahitaji kuongeza umakini wa hali ya juu zaidi.

"Simba ikienda na akili kwamba wanafungika wakiwa kwao inaweza kuwagharimu kwa sababu hata wao pia wanatambua ushindi pekee ndio utakaoweka matumaini yao hai, kikubwa ni kucheza kwa nidhamu na kutumia vizuri nafasi watakazopata," alisema.

Kwa upande wa kocha wa Simba Queens, Mussa Mgosi ambaye pia alishawahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa, alisema licha ya Wydad kupoteza michezo miwili ila Simba haipaswi kujiona ina nafasi kubwa kwani kila mchezo una malengo yake.

"Jwaneng Galaxy ilipata matokeo palepale Morocco lakini haukuwa mchezo mwepesi kwao japo lengo lao lilitimia, natarajia kuona mabadiliko ya kiuchezaji kwa Simba kuanzia kuzua na kushambulia pia kwa nidhamu kwani mchezo utakuwa ni mgumu."

Wydad inashika nafasi ya pili kwa timu iliyomiliki mpira kwani imefanya hivyo kwa 64.5% ikizidiwa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini yenye 65.3% huku ikishika pia nafasi ya pili kwa kupiga pasi sahihi kwenye mchezo mmoja kwa 430.5.

Pia timu hiyo inaongoza kwa kupiga krosi sahihi kwani imefanya hivyo kwa wastani wa 8.0 ikifuatiwa na ASEC Mimosas ya Ivory yenye 6.5 ingawa imekuwa butu kwenye kutengeneza nafasi za kufunga mabao kwani inashika nafasi ya 16 hadi sasa.

Simba inaingia katika mchezo huo wa kundi 'B ikishika nafasi ya tatu na pointi mbili baada ya kulazimishwa sare michezo miwili wakati Wydad wao inaburuza mkia kufuatia kupoteza mechi zake zote mbili huku ikiwa haijafunga pia bao lolote.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement