Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza tarehe ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba "Kariakoo Derby' kupigwa Aprili 20 mwaka huu katika Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya TPLB, leo Aprili 7 inasema "Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeupangia tarehe mchezo namba 180 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 20234\2024 kati ya Yanga na Simba maarufu kama ‘Kariakoo Derby’.

“Mchezo huo ambao haukupangiwa tarehe kwenye ratiba ilioyofanyiwa marekebisho na kutangazwa Februari 2024, sasa utachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Aprili 20, 2024 saa 11:00 jioni.”

“Klabu za Yanga na Simba na wadau wengine wa Ligi Kuu wamepatiwa taarifa zote kuhusu mchezo huo na maandalzi yake yanaanza mara moja ili kuhakikisha unafanyika katika kiwango cha juu kinachoendana na hadhi ya michezo mkubwa ya Ligi sita kwa ubora barani Afrika," taarifa imesema na kuongeza;

“Bodi ya Ligi inawatakia maandalizi mema ya wadau wote wa mchezo.”

Timu hizi zilikutana Novemba 5, 2024 raundi ya kwanza msimu wa 2023\2024 na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5 -1 katika Uwanja wa Mkapa.





You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement