Michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Dar Port Kagame Cup kuanza kutimua vumbi hii leo kwa michezo minne, Al Wadi FC dhidi ya JKU, Wanamangushi Coastal Union wakivaana na Dekedaha FC katika Dimba la KMC na SC Villa dhidi ya El Merriekh na APR FC dhidi ya Singida Big Stars wakivaana katika Dimba la Chamazi Complex Jijini Dar es salaam.

Ni timu kumi na mbili zimewekwa katika makundi matatu ambapo Timu za juu katika kila kundi na washindi wa pili watafuzu moja kwa moja kwa hatua ya nusu fainali. 

Express FC ya nchini Uganda wakiwa ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo hawapo katika sehemu ya mashindano ya kutetea ubingwa wao, Coast Union FC (Tanzania), Al Wadi FC (Sudan), JKU SC (Zanzibar), Dekedaha FC (Somalia) na Al Hilal (Sudan). 

Nao Gor Mahia FC (Kenya), Red Arrows FC (Zambia), Djibouti Telecom (Djibouti) SC Villa (Uganda), APR FC (Rwanda), Singida Black Stars (Tanzania), El Merriekh Bentiu (Sudan Kusini) wapo katika kuwania Kombe hilo.

Kumekuwa na washindi 15 wa zamani wa shindano hilo huku Simba ya Tanzania na AFC Leopards ya Kenya wakiwa na mataji mengi zaidi kwa maana ya mataji sita.

Washindi wengine ni Young Africans (Tanzania), Tusker ya Kenya wakiwa na mataji 5 kila moja. SC Villa (Uganda), APR (Rwanda), Al Merriekh (Sudan) na Gor Mahia wakiwa na mataji matatu kila moja na KCCA (Uganda) na Azam FC (Tanzania) wakiwa na mataji mawili kila moja.

Washindi wengine wote wakichukua taji hilo mara moja moja ni Express FC na Polisi ya Uganda, Rayon Sport ya Rwanda na Atraco pamoja na Vital’O ya Burundi.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement